Thursday, April 12, 2012

KARIBU KATIKA LOVE EXPRESS

  Nianze kwa kukukaribisha mpenzi msomaji kabla sijaanza kukushushia makala motomoto zinazohusu mapenzi.Kwanza ninapenda tuanze kwa kufahamu maana ya mapenzi.
  Mapenzi ni hisia za asili ambazo huchukua nafasi kutoka sehemu ya ndani kabisa ya moyo na akili ya mwanaadamu juu ya mtu au kitu chochote. Bila kusukumwa na mtu au ushawishi kutoka kwa mtu mwingine ndio maana kuna wakati unaweza kumsikia mtu akisema ``nimempenda huyu mtu hata sielewi nimempendea nini`.
Mapenzi husukumwa na hisia ,hisia ni nini?Huu ni msukumo wa vichochezi katika homoni za ndani ya mwili ambazo hutokea kutokana na mazingira husika.
Lakini huwa tofauti kati ya mtu na mtu na ndiyo maana tunatofautiana katika kupenda.

                               HUU NI MWANZO MENGI YAJA KUPITIA BLO HII.

No comments:

Post a Comment